Na. Mwandishi Wetu, Lindi
Vijana waendesha pikipik(bodaba) takriba 70, mjini Lindi jana ni kama walitia doa safari ya mtangazania kupitia chama cha mapinduzi, Edward Lowassa baada ya kuchachamaa kudaia malipo waliyohaidiwa baada ya kushiriki kikamilifu mapokezi ya mtangaza nia huyo alipokuja kusaka wadhamini katika mkoa huu.
Vijana waendesha pikipik(bodaba) takriba 70, mjini Lindi jana ni kama walitia doa safari ya mtangazania kupitia chama cha mapinduzi, Edward Lowassa baada ya kuchachamaa kudaia malipo waliyohaidiwa baada ya kushiriki kikamilifu mapokezi ya mtangaza nia huyo alipokuja kusaka wadhamini katika mkoa huu.

Wakizungumza
kwa hasira baadhi ya waendesha pikipiki hao walisema hawakubali
kudhulumiwa nguvu na muda wao kwa kutotimiziwa ahadi ya kulipwa fedha
kwakwenda kumpokea Lowassa kutoka uwanja wa ndege wa Kikwetu hadi ofisi
ya CCM mkoa wa Lindi.
"Sisi
tunataka chetu maana ahadi ni deni tulikubaliana watatuwekea mafuta lita
tatu kwenye pikipiki zetu na fedha taslimu shilingi elfu kumi" tena kwa muda wa saa moja tu, lakini tumekaa karibu saa saba hawataki kutulipa hawawezi kutudhulumu," alisikika kijana mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe.
Akieleza
kisa hicho mmoja waendesha pikipiki hao alisema wanaomunga mkono mgombea
waliwahidi kuwalipa shilingi elfu kumi nakuwawekea mafuta lita tatu
kila pikipiki iwapo watakwenda kumpokea ndugu Lowassa uwanja wa ndege wa
kikwetu ulio nje kidogo ya manispaa ya Lindi. Nakwamba makubaliano hayo
yalikuwa ni kazi ya muda wa saa moja tu. Hata hivyo walijikuta wanakaa
uwanjani hapo kwazaidi ya saa saba wakimsubiri.
Alisema ahadi ya kuwekewa mafuta ilitekelezwa lakini suala la fedha lilikuwa gumu baada ya mtangazania huyo kuondoka.
"kwakuwa
wamekiuka makubaliano tunataka shilingi elfu thelathini maana tumekaa
sana na hapa wanatupiana mpira,sasa hivi tunatoka ofisi ya CCM mkoa
tunakwenda polisi,maana kuna dada mmoja ambaye ni mpambe wake tumembana
yupo polisi"

Hali ilivyokuwa polisi.
Vijana hao
waliandamana kwenda polisi, ambako walisubiri hatma ya mdai wao wakiapa
hawatatoka eneo hilo hadi dada huyo awape pesa zao. Vijana hao wakiwa
mbali kidogo na kituo waliendelea kubaki hadi mmoja wa askari polisi wa
kituo cha Lindi alipowasihi wasifanye fujo bali wadai haki yao kwa
amani.
"Sisi
hatufanyi fujo na tumekuelewa ila tunataka haki yetu maana ni
makubaliano tunataka hela yetu na sasa dau limepanda tunataka elfu
arobaini," walisikika vijana hao.
Waendesha
pikipiki hao waliendelea kubaki kila mmoja akipaza sauti hadi
alipokwenda aliyepata kuwa mbunge wa Lindi, Abdulaziz Mohamed. Ambaye
alianza kuwauliza kimetokea nini! Nao wakamjibu wanataka pesa zao.
"Sasa
hapa polisi pana fedha zaidi ya virungu na fedha msipate! mimi
simo,ondokeni na twendeni kwa utaratibu badala ya kubaki hapa," aliwaonya.
Maneno ya
mbunge huyo yalionesha kuwaingia vijana hao ambao walikubali kuondoka
eneo hilo na kufuata hadi kwenye nyumba ambayo hadi habari hii
inaandikwa jina lake lilikuwa halijapatikana.
"Sasa tusikilizane fedha mtapata lakini kwa kwa utaratibu," alisema Abdulaziz.
Ndipo mbunge
huyo alianza kuwaita wawakilishi kwa majina ya mahali walipotokea na
kuwapatia fedha ambazo hazikuweza kufahamika ni shilingi ngapi. Ingawa
taarifa za baadae ambazo zilielezwa na vijana hao kwamba walipewa
shilingi elfu kuminatano kila mmoja.
"Tulikomaa hadi wakacheu mpunga,ila shilingi msimbazi na buku tano (shilingi 15000) lakini siyo mbaya," alisema kijana mwingine.
Dalili za
hali ya hewa kuchafuka ilianza ofisi ya CCM mkoa baada ya msafara wa
Lowassa kuondoka. Baada ya vijana hao kuanza kujikusanya nakuanza
kuhojiana hatima ya malipo yao, huku faragha za hapa na pale zikianza
kuonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni