GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumanne, 23 Juni 2015

Aunty Ezekiel: Sipendi Mwanangu Awe Mwigizaji Nataka Asome Sana

 

Staa wa Bongo Movie,Aunty Ezekiel amefunguka kuwa hapendi mtoto wake aliyejifungua hivi karibuni aitwaye Cookie,awe mwigizaji wa filamu kama yeye.
Akizungumza na Clouds Fm,alisema kuwa atakachofanya kama mzazi anataka mtoto wake asome na kama akiwa mwigizaji basi iwe kama kazi yake ya ziada siyo anayoitegemea kwenye maisha yake.

  • ‘’Binafsi sipendi mwanangu awe mwigizaji kama mimi,na siyo lazima kama mimi mama yake niwe mwigizaji na yeye awe hivyo kuna kazi nyingi ila ninachotaka asome sana na kama atataka kuwa msanii basi iwe kazi yake ya pili siyo aitegeeme katika maisha yake,’alisema Aunty.
  • ‘’Hata mimi pamoja na kwamba ni mwigizaji lakini siitegemei sana kazi hiyo nina kazi zingine nafanya,’’aliongezea Aunty.


Wema:Jamani Nikiwa Bungeni Sitaongea Hivyo na Kuropoka Kama Wengi Wanavyodai

 

Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu ambaye ametangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge wa viti maalumu Singida,amesema anafurahishwa na kitendo cha mashabiki wake kumwigiza sauti akiwa bungeni kwa  kuwa wameonyesha kumkubali kabla hajafika ‘Mjengoni’.
Alisema sauti hiyo inayomuigiza alitumiwa kupitia simu yake na haikumkwaza zaidi ya kufurahia  kwamba watu wengi wanakubali awe bungeni.


  • “Nafurahi kwa kuwa wengi wameshanipeleka bungeni wakati mimi ndiyo kwanza nipo katika harakati  za kuomba kuchaguliwa kupitia umoja wa wanawake Singida , lakini nafurahia kwa kuwa inaonyesha wengi wananikubali,  ila nikipitishwa kuwawakilisha wana Singida bungeni sitaongea kama walivyonirekodi katika sauti hiyo,” alisema Wema kwa furaha.

Baraza kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA) lamteua Sheikh Aboubakar Zuberi kuwa Mufti mpya

 

Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limemteua Sheikh Aboubakar Zuberi kuwa Mufti Mpya wa muda.

Sheikh Zuber atashikilia nafasi hiyo kwa muda wa miezi mitatu (siku 90) kuelekea katika uchaguzi wa kumpata atakayerithi nafasi hiyo kwa mamlaka kamili.

Video ya Interview ya Wema Sepetu Kuhusu Mtoto na Diamond, Mimba ya Zari na Alivyotoa Mimba

 
'Kukosa mtoto wakwangu inaniuma naishia kupenda watoto wa watu'- Wema

Hii  ni Part iv  ya Wema Sepetu aliyofanya katika kipindi cha Take One na Zamaradi , kafunguka mambo mengi na kumuongelea Zari .


Jack Patrick Akirudi, Vanessa Atakuwa na Nafasi Kwa Jux?

 

Super model ambaye yupo gerezani kwa sasa kutokana na ishu ya kukamatwa na madawa ya kulevyia nchini China Jack Patric .

Awali mwana dada huyo aliwahi kuwa na mahusiano yakimapenzi na mwanamuziki wa bongo fleva Juma Jux ,lakini baada ya mwanadada huyo kutupwa garezani kwa miaka kumi ,Jux ameamua kunzisha mahusiano na Vanessa Mdee  huku wakiwa wanaponda raha za  kufa  mtu. .

Awali jux alinukuliwa na kituo kimoja cha redio kuwa hatakama mpenzi wake Jack yupo jela ila bado atalilinda penzi lao mpaka akaamua kumtungia nyimbo ‘’Nitasubiri’’

Je, Jux ameamua kumsaliti Jack nakuwa na Vanessa au kaona soo kuwa na Jack kisa kapatwa na skendo hiyo??? Jack akitoka jela atakuwa ana nanafasi gani kwa jux au Vanessa atapigwa chini ???

Jack awalii aliwahi kuolewa na  mwanume afahamikaye kwa jina la  Fundikila lakini ndoa yao  ilivunjika kutokana na  mwana dada huyo kumsaliti mumewe kwa Jux hadi kupelekea kila mtu kushika time yake .

Je kwa hali ya kawaida Jux ameonyesha kutokuwa mvumilivu nakuvunja ahadi au yupo na Vanessa kwa short time ???

Funguka 

Jumatatu, 22 Juni 2015

MPIGIE KURA VANESSA MTV MAMA 2015

Sugu Amfikisha Mkewe Kortini..Kisa Kuvaa Nusu Utupu na Kupiga Picha za AIBU

 

KINDUMBWENDUMBWE! Mbunge wa Mbeya Mjini kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’ amemfikisha kortini aliyekuwa mkewe,  Faiza Ally akitaka apewe mtoto wao, Shaa (2) ili amlee kwa vile mama yake huyo si mwadilifu.

Aliyekuwa mkewe na mbunge wa mbeya mjini Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’,  Faiza Ally akiwa katika pozi.

Ijumaa iliyopita, saa 2:00 asubuhi, Faiza alipanda kwenye kizimba cha Mahakama ya Mwanzo, Manzese/ Sinza iliyopo Sinza-Makaburini jijini Dar kwa ajili ya kukabiliana na madai hayo.

 Alieyekuwa mke wa mbunge wa mbeya mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" akiingia mahakamani.

ZILIPO HASIRA ZA SUGU

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichomwaga ‘ubuyu’ huo, Mheshimiwa Sugu alifikia hatua hiyo baada ya kuchukizwa na tabia mbaya za mwanamke huyo hasa ya kuvaa nguo zinazomuacha nusu utupu na kupiga picha za aibu, akiamini kuwa, tabia hizo zinaweza kuathiri makuzi ya mtoto huyo.

Mnyetishaji huyo aliendelea kusema kuwa, kwa kipindi kirefu, Sugu amekuwa akimvumilia Faiza, lakini hivi karibuni uzalendo ulimshinda baada ya picha zake akiwa amevaa kigauni kifupi na makalio nje kusambaa mitandaoni.

PALIPOKOLEZEA HASIRA

Faiza alivaa kivazi hicho hivi karibuni kwenye hafla ya ugawaji wa Tuzo za Kili Music iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City, Dar.

 SUGU MBELE YA HAKIMU

Akizungumza mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Patrick Vaginga, Mheshimiwa Sugu alidai kuwa mbali na mzazi mwenzake huyo kuwa na tabia ya kuvaa nusu utupu pia ana mtindo wa kupiga picha zisizo na maadili na kuziweka mtandaoni yeye mwenyewe.

 Joseph Mbilinyi akionekana kwa mbali katika maeneo ya mahakama.

KUHUSU MTOTO

Sugu alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, pia mwanamke huyo amekuwa na tabia ya kumpiga picha mbaya mtoto wao na kuzimimina humohumo mitandaoni jambo ambalo alisema linamharibu mtoto huyo.

 FAIZA HANA PESA

Mbali na sababu hizo, pia Sugu aliongeza kuwa, Faiza hana kipato kizuri cha kuweza kumlea mtoto na mara kwa mara amekuwa akisafiri jambo ambalo husababisha mtoto huyo kutopata malezi ya mama kwa muda mrefu hivyo kuiomba mahakama impe haki yeye ya kuishi na mwanaye.

 FAIZA AJIBU MAPIGO

Naye Faiza akijibu mapigo katika utetezi wake alisema kuwa, Sugu hafai kumlea mtoto huyo kwa sababu naye ana tabia ya kusafiri kwa muda mrefu hivyo kuishi mbali na mtoto ambapo aliiomba mahakama hiyo isimruhusu baba mzazi huyo kuishi na mtoto kwa kuwa atamharibu.

KESI YAPIGWA KALENDA

Mheshimiwa Hakimu Vaginga akasema kwa vile kesi hiyo ndiyo imeanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza aliiahirisha hadi baadaye mwezi huu ambapo hukumu itatolewa.

 SUGU NJIA YAKE, FAIZA NJIA YAKE

Ijumaa Wikienda lililokuwa mahakamani hapo, liliwashuhudia wazazi hao, kila mmoja akiondoka na njia yake.

KWA NINI FAIZA NI MKE WA SUGU?

Kwa sheria za Kitanzania, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita, hao tayari ni mke na mume kama ilivyokuwa kwa Faiza na Sugu ambao waliishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili.

Makongoro Nyerere Ametumwa na Nani Urais 2015?


 Hakuna kipindi ambacho CCM imeingia katika Uchaguzi Mkuu ikiwa na makundi hatarishi na pia matatizo ya kiutawala kama uchaguzi Mkuu ujao.

Ujio wa Abdulrahman Kinana kama Katibu Mkuu kwa kiasi kikubwa umekichelewesha chama kumeguka vipande vipande kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao.

Wataalam wa kisiasa wanaendelea kujiuliza maswali mengi kuhusu hatima ya makundi na uhasama unaorutubika kila siku ndani ya CCM.

Udhaifu wa viongozi wakuu wa chama umesababisha baadhi ya wanachama kufanya watakacho kwa kukiuka kanuni, maadili na taratibu za chama mpaka kufikia hatua ya kutaka kumuondolea Rais Kikwete kofia ya Mwenyekiti wa CCM-Taifa.

Kuibuka kwa Makongoro Nyerere katika kundi la wanachama ambao wanaomba kuteuliwa kuwa wagombea Urais wa Tanzania kumeufanya uwanja wa siasa ndani ya CCM kubadilika hasa ikichukuliwa kuwa, hakuna mwanaCCM ambaye alikuwa akiongea na kusikilizwa kwa makini na wanachama wa CCM kuhusu kile kilichokua kinaendelea ndani ya CCM.

Makongoro amewashambulia vikali baadhi ya watia nia kama Edward Lowassa, Mwigulu Nchemba na Stephen Wasira kama ndiyo baadhi ya wale wanaleta maradhi ndani ya CCM pamoja na kwamba CCM bado ni chama bora nchini.

Pamoja na mambo mengine, Makongoro aliwatuhumu kwa kuja na Ilani yao ya uchaguzi badala ya kusubiri Ilani ya CCM itakayopitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM-Taifa.

Alisema ndani ya chama hicho kumekuibuka pia genge la watu wachache ambao utajiri wao ni wa shaka na umejijenga kwa fedha chafu.

“Ndani ya chama tawala wamekuwapo ‘vibaka’ wachache… unajua kibaka ni kibaka tu hata kama kapewa gari la Serikali lina bendera ya taifa mbele atabaki kuwa kibaka tu. Hawa ndiyo wanaotuvurugia chama na hawamheshimu Mwenyekiti wa chama, Rais Jakaya Kikwete’’, Makongoro alisema.

Makongoro ameamua kuchukua jukumu la viongozi wakuu wa CCM ili kupambana na makundi yanayohatarisha uwepo wa CCM katika uwanja wa siasa.

Sauti ya Makongoro ukiichunguza kwa makini ni kama sauti ya mtu aliaye nyikani!

Kwa sauti hii, ni nani amemtuma Makongoro ili kupambana na wanachama anaowaita ni vibaka wanaosababisha baadhi ya viongozi wa CCM kuishi maisha ya kusukumwa kwa upepo wa makundi yanayomilikiwa na watoa fedha.

Je, inawezekana sauti ya Makongoro ni sauti ya viongozi wakuu wa CCM?


Makongoro atauweza mfupa uliowashinda viongozi wakuu wa CCM?.

ALI KIBA Atangaza Vita na Mwanamuziki Diamond Platnumz

 

VITA! Saa chache tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar akitokea nchini Marekani kwa shughuli za kimuziki, staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ametangaza kile kinachotafsirika kuwa ni vita dhidi ya hasimu wake kwenye anga la muziki huo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ijumaa Wikienda lina ‘full’ stori.
 cdeaw3
TUJIUNGE ENEO LA TUKIO

Ali Kiba alitema cheche Alhamisi ya wiki iliyopita ndani ya Hoteli ya Sea Cliff, Masaki jijini Dar, kulikokuwa na uzinduzi wa kampeni ya kupinga vita ujangili, iliyoratibiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, huku akiwa ni mmoja wa mabalozi sanjari na mlimbwende wa zamani, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi ‘K-Lyin’.


USO KWA USO NA PAPARAZI

Baada ya shamrashamra za ‘event’ hiyo, haraka sana kama mshale wa Mmakonde, mwandishi wetu alimfuata Ali Kiba, lengo kuu likiwa ni kusikia chochote juu ya ushindi wa Tuzo za Kili ambapo alizoa tano binafsi na moja ya kushirikishwa.

Kiba alisema anaamini alistahili kushinda tuzo zote kwani vigezo na sifa anazo na amejiandaa kikamilifu kupambana na yeyote anayedhani kuwa ni mfalme wa muziki huo.

JINA LA DIAMOND LAMCHEFUA!

Katika mahojiano hayo, mwandishi wetu alimkumbusha Ali Kiba uwepo wa Diamond ambapo kwa haraka sana alimkata kauli mwandishi kwa kusonya na kuweka wazi kuwa miongoni mwa mambo ambayo humpa kichefuchefu, ni pamoja na kusikia jina la Diamond likitajwa mahali popote penye uwepo wake!

“Kaka, sitaki kabisa kulisikia jina hilo, linanipa kichefuchefu, unajua kwa kipindi ambacho nilikaa kimya, nilikuwa nausoma mchezo lakini hakuna aliyeweza kuchukua kiti changu na kuamua kurejea ulingoni kwa kishindo na kuanzia sasa hivi ni mapambano mwendo mdundo,” alisema  Kiba na kuongeza:

“Simaanishi kuwa hakuna msanii mzuri kama mimi, naomba nisieleweke vibaya, wapo lakini siyo huyo dogo (Diamond), muziki ni zaidi ya mbwembwe, niko kikazi na sasa nimedhamiria kweli, kama anaamini yuko fiti, kazi zitaweka wazi ukweli na si drama za kitoto.”

 VIPI KUHUSU YEYE NA WEMA?

Mwandishi wetu alitaka kujua kulikoni msanii huyo alimuweka Wema Sepetu kwenye ukurasa wake wa Instagram akimmwagia shukrani lukuki na si mtu mwingine?

“Wema amekuwa ni shabiki wangu wa siku nyingi mno, alianza kunipenda kupitia wimbo wangu wa Hands Across the World (kwenye Project ya One-Eight) na kuanzia hapo amekuwa akinipa sapoti kubwa sana, siwezi kukaa naye mbali eti kisa huyo jamaa (Diamond).

“Naamini kwa asilimia nyingi sana hata huu ushindi wangu wa tuzo, umechangiwa na sapoti yake pamoja na wadau wangu wengine,” alisema Kiba.

 AFUNGUKA KUHUSU VIDEO YA MWANA!

Pia, mwandishi wetu alimtaka staa huyo kufafanua madai ya kutoitendea haki video ya Wimbo wa Mwana, ambapo alisema, watu wengi walitarajia aifanye kulingana na mawazo yao ndiyo maana akaamua afanye vile anavyoaamini ingekuwa bora.

“Kila mtu alikuwa ameshatengeneza picha ya jinsi video ya wimbo itakavyokuwa, halafu sifanyi kazi kwa kushindana na mtu, ndiyo maana ilionekana tofauti na mawazo ya wengi, namalizia kwa kusema salamu zimfikie jamaa (Diamond) kuwa mapambano ndiyo kwanza yameanza,” alisema Kiba.

 DIAMOND ANASEMAJE?

Hadi tunakwenda mitamboni, jitihada za kumpata Diamond aweze kuzungumzia vita hiyo iliyofufuka upya hazikuzaa matunda kufuatia simu ya staa huyo aliyekuwa nchini Afrika Kusini kikazi, kuita bila majibu.

 TUJIKUMBUSHE

Kwa muda mrefu sasa, Kiba na Diamond wamekuwa wakiripotiwa kuwa na bifu la chini kwa chini linalotokana kugombania ufalme wa muziki Bongo. 

Zitto Awapiga Dongo CCM ..Adai Hawaaminiani wala Kuthaminiana Wenyewe kwa wenywe

 

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe, amesema utitiri wa wagombea urais kupitia CCM kunaonyesha dalili ya wao wenyewe kutoaminiana, kutothaminiana na kimepoteza hazina ya viongozi.

Aidha, alisema kazi ya urais ingekuwa inachukuliwa kwa uzito wagombea wa CCM wasingefikia 10 badala yake imeonekana nikazi nyepesi na imerahisishwa na CCM.

Kabwe alisema sifa 13 pekee za wagombeawa CCM ni nyepesi ndio maana kila mmoja anajiona anaweza kuwa kiongozi wa nchi.

Akizungumza jana mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, Kabwe alisema moja ya sifa ya chama cha ACT-Wazalendo ni wagombea kufuata masharti kwa kutangaza mali na madeni ikiwamo kufuata miiko ya viongozi iliyotangazwa na Azimio la Tabora.

Kabwe aliwataja viongozi hao kuwa ni wa kitaifa wa chama, rais, mawaziri, wabunge na madiwani watakaotokana na chama hicho.

Aliongeza kuwa ili kubomoa mfumo wa kinyonyaji na kifisadi miongoni mwa viongozi, chama hicho kimeamua kurejesha miiko ya uongozi na kuishia ambayo imehusishwa kutokana na Azimio la Arusha.“Chama kinamtaka kiongozi katika uongozi wa umma asiwe mkurugenzi katika kampuni au shirika la umma, awe wazi na vyanzo vyake vya mapato, mali alizonazo kwa kuzingatia utaratibu wa sheria ya nchi na kanuni za mwenendo na maadili ya viongozi,” alisema Kabwe.

Pia, alisema kiongozi anatakiwa asiwe mfanyabiashara wa aina yoyote katika chama na serikali anapokuwa kwenye nafasi ya uongozi.

Alisema tangu wagombea hao waanze kutangaza nia hakuna mgombea urais aliyetamka neno miiko isipokuwa Samuel Sitta pekee, licha ya kuahidi kupambana narushwa pamoja na ufisadi.“Nitolee mfano nchi ya Canada, Uingereza, Marekani wana miiko lakini Tanzania tunageuza uongozi kuwa kichaka cha wezi kwa kutupa miiko pembeni,” alisema Kabwe