Mama na Mtoto
AMA kweli ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni! Msemo
huu unakwenda sambamba na tukio la hivi karibuni la mkazi mmoja wa Kijiji cha
Nghoboko wilayani Meatu mkoani hapa, Stephano Mihilu mwenye miaka 60, kudaiwa
kumfumania mkewe wa ndoa akifanya mapenzi na mtoto wao wa kumzaa. Taarifa za
kipolisi zilizotua kwenye dawati la Waandishi zinadai kuwa tukio hilo la aina
yake lilitokea usiku wa Julai 22, mwaka huu ambapo baada Stephano kulishuhudia
tukio hilo, aliwaua mama na mwanaye kwa kuwacharanga mapanga bila huruma.
“Jamaa aliporudi nyumbani, aliingia ndani na kukutana na tukio ambalo hakuwahi
kulifikiria, alimkuta mkewe akifanya mapenzi na mtoto wao wa kumzaa, nadhani
akili ilihama, akachukua panga na kuwacharanga wote mpaka walipokata roho,”
alisema afande mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwani si
msemaji wa jeshi la polisi.
HUYU HAPA KAMANDA WA POLISI WA SIMIYU Akilizungumzia tukio
hilo la kusikitisha na kushangaza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Afande
Salum Msangi aliwataja waliouawa kuwa ni Kundi Sita mwenye umri wa miaka 40,
ambaye alikuwa mkewe na Boyani Stephano mwenye miaka 27 ambaye ni mtoto wao wa
kumzaa. Alidai kuwa, Mihilu alimkuta mkewe akifanya tendo la ndoa na mtoto wake
wa kumzaa ndipo alipopandwa na hasira kisha kuwashambulia kwa kuwakata mapanga
na baadaye kuwachinja. Kamanda Salum alisema, baada ya mauaji hayo, mtuhumiwa
huyo alikwenda mwenyewe kujisalimisha kwenye kituo cha polisi ambapo alikabidhi
silaha alizotumia katika mauaji hayo ambazo ni panga na fimbo. “Mihilu
alitembea kuanzia saa 7 usiku hadi asubuhi kwenda katika Kituo cha Polisi cha
Mwahuzi wilayani Meatu kwa lengo la kujisalimisha akidai kuwa hakutaka
kuwasumbua wanausalama hao kwani yeye ndiye mhusika wa mauaji hayo,” alisema
kamanda huyo.
WANANCHI
WANALIZUNGUMZIAJE TUKIO HILO? Wakizungumza na mwandishi wetu baada ya tukio
hilo, baadhi ya wananchi wameonesha kushangazwa nalo huku wakieleza kuwa, kama
ni kweli basi dunia inaelekea mwisho. “Hivi inawezekanaje mama kufanya tendo la
ndoa na mwanaye wa kumzaa? Au kuna mazingira ya ushirikina?” alihoji Juma
Sagala wa Meatu. Naye Mama Josephine, mkazi wa kijiji ambacho tukio hilo
lilitokea alisema: “Hili tukio lina utata lakini kwa kuwa limeshafika kwenye
vyombo vya dola, ukweli utajulikana na sheria itachukua mkondo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni