Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma akiongea na waandishi wa habari Jumanne hii
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma, amesema zoezi hilo litasaidia kupata taarifa sahihi za watumiaji wa simu nchini.
“Sasa hivi zoezi litakuwa kiteknolojia zaidi. Utakuwa ukipigwa picha na simu. Kwahiyo uso huwezi ukafeki,” amesema Profesa Nkoma.
Ameongeza
kuwa zoezi hilo litasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa udanganyifu
uliopo kwenye matumizi ya simu nchini na hakutakuwa na urahisi wa mtu
kutumia jina la bandia pamoja na picha isiyokuwa yake.
Profesa
Nkoma amesisitiza kuwa zoezi hilo halimaanishi kuwa ni usajili mpya wa
sim card bali ni uhakiki wa taarifa za watumiaji wa simu nchini na
linamhusu kila mmoja.
Kwa
upande wake Rene Meza ambaye pamoja na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom
Tanzania, ni mwenyekiti wa chama cha watoa huduma za mawasiliano nchini,
MOAT alisema zoezi la usajili wa simu nchini limeingia kwenye hatua
nyingine ya juu zaidi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Vodacom Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha watoa
huduma za mawasiliano nchini, MOAT akiongea na waandishi wa habari
“Ni
kwa kutumia teknolojia, na tena ni kwa smartphone ambayo wakala wa
usajili ataipata kwa si zaidi ya shilingi laki moja ambayo itamsaidia
kuchukua picha ya mteja anayetaka kusajili sim card yake. Mchakato huo
hutumia zaidi ya dakika tano,” alisema Meza.
Meza amesema
usajili huo utafanyika nchi nzima na wameifanyia uhakiki teknolojia
hiyo kwa zaidi ya miaka mitatu na tayari kuna vituo zaidi ya 5000
vinavyofanya usajili huo mpya.
Wateja watatakiwa kuonesha vitambulisho vinavyokubalika kufanikisha zoezi hilo na utagharimu shilingi 1000 tu.
Kwa upande
wake mamlaka ya vitambulisho nchini, NIDA, imedai kuwa vitambulisho vya
uraia vitalazimika kutumika zaidi ili kupata taarifa sahihi za watumiaji
wa simu.
NIDA
imesema imeboresha pia utoaji wa vitambulisho hivyo kwa Dar es Salaam
ambapo wananchi wakiwasilisha viambatanisho vinavyotakiwa watakuwa
wakivipata ndani ya siku 7.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni