Kila mmoja anatambua kuwa elimu haina
mwisho na kadri miaka inavyokwenda watu wengi wamekuwa wakitambua nini
maana ya elimu huku wengi wao wakiamua kurudi darasani ili kujiongezea
ujuzi zaidi.
Kila mmoja anatambua kuwa elimu haina
mwisho na kadri miaka inavyokwenda watu wengi wamekuwa wakitambua nini
maana ya elimu huku wengi wao wakiamua kurudi darasani ili kujiongezea
ujuzi zaidi.
Unamkumbuka yule kikongwe wa miaka 90 Priscilla Gogo
huko Kenya aliyekuwa akisoma darasa la tano na wajukuu zake sita?
aliaminika ndiye mwanafunzi mzee zaidi duniani kusoma shule ya msingi.
Priscilla Gogo
Ukiachia stori hiyo wiki chache
zilizopita huko Ujerumani kikongwe wa miaka 102 alihitimu PHD yake ya
udaktari, Leo tena nimekusogezea ya bibi huyu Doreetha Daniel aliyemaliza degree yake kwenye chuo cha Canyons huko Santa Clarita, Carlifonia.
Akiwa na miaka 99 alianza safari yake ya elimu mwaka 2009 na kupania kupata degree yake kabla ya kutimiza miaka 100.
Bibi huyo amevunja rekodi katika chuo hicho kwa kuwa mwanafunzi mzee zaidi tangu kuanzishwa kwa chuo hicho miaka 45 iliyopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni