Nimekurekodia Uchambuzi wa stori za magazetini zilizosikika juzi tarehe 10/06/2015 redioni @CloudsFM.
Idadi ya waliotangaza Kugombea Urais kupitia chama cha CCM yafikia 22, yuko January Makamba, Balozi Amina Ali Salum, Bernard Membe, Makongoro Nyerere, Edward Lowassa, John Magufuli, Lazaro Nyalandu na Samuel Sitta.
Ishu nyingine ni hukohuko kwenye Uchaguzi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda yeye kutangaza nia ya Ijumaa wiki hii, Waziri Mathias Chikawe nae atatangaza nia ya kugombea Urais leo.
Magazeti yameandika pia maswali makubwa
nane muhimu yaliyowakimbiza wagombea Urais katika mdahalo uliofanyika
tarehe 08, Mdahalo mwingine umepangwa kufanyika tarehe 18 na 25 mwezi huu.
Stori nyingine ni kutoka Njombe ambako
watu 100 watafikishwa mahakamani na tume ya uchaguzi wa Taifa kwa
kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye daftari la wapigakura.
Unaweza sikiliza stori hizi za leo katika audio hii nliokurekodia hapa chini mtu wangu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni