Zimepita kama saa 48 tu toka Timu ya Yamoto Band
ipae toka Uwanja wa Ndege wa JNIA Dar es Salaam kuelekea South Africa
kwa kazi moja tu, kuandaa video yao ambayo wanaifanya na Director Godfather.
Picha ya kwanza ilionesha wako meza moja na Director huyo, alafu pembeni alikuwepo Diamond Platnumz pamoja na Mkubwa Fella na Babu Tale pia.
Post imepanda muda mfupi uliopita kwenye page ya Diamond @Instagram ikionesha tayari kazi imeanza… unaweza kucheki hapa kipande cha video hiyo Yamoto Band wakiwa Location.
Tunazijua kazi nzuri za Yamoto Band na tunaijua kazi nzuri pia ya Godfather, tukae tayari kwa kila kizuri kitakachotokea huko mtu wangu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni