Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa mambo ya Nicki Minaj utakua umeshaona zile post za Twitter za majibishano kati ya Nicki Minaj na ex-boyfriend wake Safaree Samuels siku
chache zilizopita. Lakini inawezekana kuna kitu ulikua hukijui kuhusu
ex-couple hii. Kwenye interview alioifanya kipindi cha hapa nyuma Nicki alisikika akisema maneno haya kuhusu ex-boyfriend wake.
>>>> “Unajua
nini, kama nisingekua rapper, leo ningekua nimeolewa na nimezaa nae
watoto, na najua mimi kua msanii mkubwa leo kumesababisha vitu vingi
viharibike hata yeye anajua..na inaniuma, unajua kwa sababu gani?…
Umaarufu ni kitu kibaya sana, kwasababu nimeona uchu wa mtu (hata mimi)
kutaka kua maarufu kuharibu vitu fulani katika maisha haswa katika
mahusiano ya kimapenzi na sana sana kama mlikua tayari mnafocus yenu ya
maisha..!!”
>>>> “kanifanyia
mengi sana kimaisha na kimuziki. Nataka watu wanielewe hapa, nimekua
nae kwa muda mrefu sana hata kabla ya umaarufu. Sometimes natamani
kumwambia vitu ambayo nahitaji mawazo yake tuu na sio ya mtu mwengine
lakini nashindwa… hio inaniumiza! Hakua tuu boyfriend kwangu..no! Alikua
sehemu ya maisha yangu. Na licha ya mimi kuendelea na maisha yangu,
sometimes inaniwia vigumu kumudu vitu fulani kwa sababu najikuta sijui
jinsi ya kukaa na mtu kama nilivyokua nae, so siwezi kukaa hapa na
kujifanya kama hakua kila kitu kwangu no..I loved him, he was my world
na bado yupo moyoni!”
Kwa sasa Nicki Minaj
ameamua kuendelea na maisha na amesema kua ana furaha na amani japo sio
rahisi wakati mwengine, ila kwa yote yeye bado anamshukuru mungu.
Anampenda Meek Mill na hajui watafika mbali kiasi gani ila anatumaini watakaa kwa muda mrefu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni