Member wa kundi la Navy Kenzo
ambaye pia ni mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka 2015, Nahreel
amefunguka kuwa kupelekea kufanya vizuri kwa single zinazojulikana kama Nana ya Diamond Platnumz na Nusu Nusu ya Joh Makini ameanza kupata mafanikio nje ya Tanzania.
Akizungumza na millardayo.com alisema..’Kwanza
nawashukuru watu kwa kunipigia kura na kuniwezesha mimi kuwa producer
bora wa mwaka, na kwa upande wa kazi zipo nyingine zinakuja kuna kazi ya
Joh Makini na rapper kutokea Afrika Kusini AKA, Vanessa Mdee nyingine ya Ben Pol kwa hiyo kuna kazi nyingine zinakuja kutoka nje ya Tanzania
Tangu nilipotengeneza wimbo wa Nana ya Diamond
na Nusu Nusu ya Joh Makini nimeanza kupokea connection mbalimbali
kutoka Nigeria na sehemu mbalimbali kwa mfano Vanessa Mdee pia ametoka
kuniambia kuwa Yemi Alade kuwa anataka kufanya kazi na mimi chini ya The
Industry Studio kwa hiyo mashabiki wa Nahreel wakae tayari kwa muziki
mzuri…”alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni