Wapelelezi wanaofuatilia kashfa ya rushwa inayohusu shirikisho la
soka ulimwenguni FIFA wameahidi kufichua makubwa zaidi baada ya kugundua
siri nzito zilizojificha kwenye mchakato wa kuchagua mwenyeji wa kombe
la dunia.
Wapepelezi hao wakiongozwa na Mwanasheria mkuu wa Uswissi Michel
Lauber wamesema kuwa kuna matukio karibu 53 ya uchakachuzi na
utakatishaji haramu wa fedha ambayo yamegundulika kwenye michakato
tofauti ya kumpata mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia na matukio
haya yamehusishaa watu wazito ambao kama yatagundulika undani wake
yatazua hofu na utata mkubwa .
Mwanasheria mkuu nchini Uswissi Michel Lauber akizungumza na waandishi wa habari.
Mwanasheria huyo ameonya kuwa hatajali kama upelelezi wake
utasababisha hasara ya fedha au kupokonywa uwenyeji kwa nchi za Urusi
na Qatar na anachojali ni ufanisi wa kazi yake na si kitu kingine .
Imedaiwa kuwa upelelezi huu uahusisha kuhojiwa kwa viongozi wa juu wa
Fifa akiwemo rais wa zamani Sepp Blatter ambaye hivi karibuni
alitangaza kujiuzulu siku chache baada ya kuchaguliwa kwa kipindi cha
tano .
Rais wa Fifa wakati akitangaza mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 .
Viongozi kadhaa wa zamani wa Fifa wakiwemo Mmarekani Chuck Blazer na
rais wa zamani wa chama cha soka cha Trinidad and Tobago Jack Warner
wameahidi kutoa ushirikiano kwa wapelelezi huku wakiahidi kuwa
watazungumza bila kuficha .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni