Baada ya Barcelona kutwaa mataji matatu
ya La Liga, Copa de Rey na ligi ya mabingwa Ulaya sasa wamekuja na
mikakati yao tayari kwa ajili ya msimu mpya.
Tayari Barcelona imesaini mkataba mwingine mpya na Kocha wake, Luis Enrique, ambao sasa utaisha mwaka 2017.
Kabla ya hapo, Barcelona ilimuongezea mkataba wa mwaka mmoja beki wake
Dani Alvez pia ikamsajili beki mpya Aleix Vidal ili kuisaidia timu hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni