Kama hukusikiliza Hekaheka ya leo Jan 15 inatokea Kunduchi, Dar inahusu mama ambaye inasemekana amekuwa akimtesa mtoto wake kwa kumpiga kitendo kilichowachosha majirani na kuamua kumchukua mtoto huyo.
Mtoto huyo amesema kuwa mama yake amekuwa akimpiga kwa banio la kupikia ugali, chupa na waya ambapo mara ya mwisho alimpiga kwa kumtuhumu kumuibia fedha baada ya kumtuma dukani.
Mama huyo alipoulizwa amesema mtoto huyo alikuwa na tabia za ajabu toka akiwa mdogo na amekuwa akimpiga kwa fimbo ili ajirekebishe japo majirani hawakukubaliana na utetezi wa mwanamke huyo.
Baba ambaye ni jirani aliyemchukua mtoto huyo amesema tayari amepeleka suala hilo Polisi na amepeleka barua kwa mjumbe ili aweze kukaa na mtoto huyo kwa kufuata utaratibu unaotambulika.
Unaweza kusikiliza hekaheka hiyo kwa kubonyeza play.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni