GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumamosi, 6 Septemba 2014

"SIJAACHANA NA MKE WANGU LAD JAY DEE, TUPO VIZURI SANA TU" ADAI GADNER G HABASH

Gardener G Habash azungumzia tetesi za kuachana na Lady Jay Dee na chanzo chake,
Gardner G Habash amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kwenye mitandao kuwa yeye na mkewe Lady Jay Dee wako kwenye wakati mgumu wa ndoa yao.

Akizungumza katika Exclusive Friday ya 100.5 Times Fm, Gardner ameeleza kuwa hizo ni taarifa zisizo za kweli ambazo amekuwa akizisikia tu.

“Hakuna tatizo. Kusema ukweli nimekaa na Lady Jay Dee kwa miaka mingi sana na hii sio mara ya kwanza kuzungumzwa kwa mambo kama hayo. Na tumeshazoea. 

Hata kama kuna kitu kinazungumzwa, mimi hata sina habari kwa sababu nimeshazoea. Kwa hiyo na mimi pia nimesikia kama ulivyosikia wewe. Lakini tatizo hakuna.” Amesema Gadner.

Ameeleza kuwa chanzo cha tetesi hizo kinaweza kuwa siku ambayo yeye alionekana polisi  katika kesi ya usalama barabarani na Lady Jay Dee hakufika.

Amesema huenda watu walichukulia tofauti lakini ukweli ni kwamba yeye ndiye aliyemshauri asiende ili kuepusha attention zaidi.

“Na kwa watu kuzungumza…unajua Jay Dee ni mtu mashuhuri, ni mkubwa sana. Kiasi kwamba kitu kidogo tu kikitokea, hata akijikwaa kinazungumzwa kwa ukubwa huo.

 Kwa mfano mimi nimepata shida kidogo ya kesi ya traffic, kwa hiyo nikamshauri mwenzangu asije pale polisi kwa sababu ya kuogopa tu vitu kama mapicha na nini. Kumbe watu walinotice kwamba hakuja. 

Kuanzia hapo ndio ikaanza ‘aah kuna tatizo..kuna tatizo’. 

“Lakini kwa kweli kuzungumzwa kwa msanii mkubwa kama yule ni jambo la kawaida. Na ni jambo ambalo ameshalizoea na mimi nimeshalizoea pia.” 

Hivo karibuni Jide alipost picha ya mkono inayoonesha pete yake ya ndoa kumaanisha uimara wa ndoa yao tofauti na kilichokuwa kikisemwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni