GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumatatu, 18 Agosti 2014

Sheikh Juma Ngao wa Kenya azungumzia sababu za vijana kujiunga na makundi ya kigaidi


Nchini Kenya, tatizo la ukosefu wa ajira na ugumu wa maisha katika eneo la Pwani ni mambo yanayotajwa kuwa yanawasukuma vijana wengi kujiunga na makundi ya kigaidi kama al-Shabab au kundi linalopigania kujitenga eneo la Pwani la MRC. Juhudi mbalimbali zinafanyika ikiwa ni pamoja na kuitishwa makongamano ya kutoa elimu kuhusiana na maana halisi ya jihadi ambayo inapotoshwa na baadhi ya makundi yasiyoufahamu vyema Uislamu. Kujadili suala hilo, Salum Bendera amezungumza na Sheikh Juma Ngao Mwenyekiti Taifa wa Baraza la Ushauri wa Kiislamu nchini Kenya KEMNAC ambaye kwa kuanzia anaelezea iwapo sababu inayotolewa ya vijana kujiunga na makundi ya kigaidi kama kweli ni ya kukubalika au la.

-IRIB

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni