Watu waliokuwa na silaha waliokuwa wakidai kuwa hakuna mripuko wa homa hatari ya ebola huko Liberia usiku wa kuamkia leo wamekivamia kituo kimoja cha karantini kilichokuwa na wagonjwa wa ebola huko Monrovia mji mkuu wa nchi hiyo na kusababisha wauguzi na wagonjwa wasiopungua 20 kukimbia.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo anayejulikana kwa jina la Rebecca Wesseh ameeleza kuwa, watu hao walivunja mlango na kuiba vitu kadhaa katika kituo hicho.
George Williams Mkuu wa Jumuiya ya wafanyakazi wa sekta ya afya ya Liberia amesema kwamba kituo hicho kilichokuwa kikiwahifadhi watu walioambukizwa homa hatari ya ebola kilikuwa na wagonjwa 29 ambao walikuwa wakipatiwa matibabu ya awali kabla ya kupelekwa hospitalini. Amesema wagonjwa hao wote walikuwa wamebainika kuwa na virusi vya ebola.
-IRIB
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni