GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumatatu, 18 Agosti 2014

Borno na Adamawa wawakimbia Boko Haram

Wakazi wa majimbo ya Borno na Adamawa huko Nigeria wamezikimbia nyumba zao kufuatia kuchapishwa taarifa za kutatanisha kwamba kundi la wanamgambo wa Boko Haram limejianda kuyashambulia maeneo hayo. 

Robin Abati Msemaji wa wa Rais wa Nigeria katika masuala ya habari ameeleza kuwa taarifa zilizoenea kwamba kundi la Boko Haram limejitayarisha kufanya mashambulizi katika maeneo kadhaa ya majimbo ya Borno na Adamawa huko kaskazini mashariki mwa Nigeria zimezusha hofu na wasiwasi miongoni mwa wenyeji wa maeneo hayo.

Robin Abati ameongeza kuwa baadhi ya wakazi wa majimbo hayo wamezikimbia nyumba zao na wakazi wengi  wa vijiji vya Borno  wamekimbilia katika jimbo la mji wa Maiduguri wakihofia mashambulizi ya Boko Haram. Hii ni katika hali ambayo Mkurugenzi wa itelijensia ya taifa jana alitangaza kuwa maafisa usalama wa nchi hiyo wamewatia mbaroni wanawake wawili wanachama wa kundi la kitakfiri la Boko Haram huko katika mkoa wa Katsina kaskazini mwa Nigeria, ambao walikuwa na lengo la kutekeleza oparesheni ya uharibifu.  

-IRIB

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni