Uingereza inatarajia kuufunga Ubalozi wake kwa muda atika mjii mkuu wa Tripoli nchini Libya kufuatia mapigano makali katika mji wa Benghazi. Zaidi ya watu mia mbili wameuwawa katika miji hiyo miwili katika kipindi cha majuma mawili yaliyopita.
Wizara ya maswala ya kigeni nchini Uingereza imesema kuwa opareshioni ya za Ubalozi huo zittsitishwa baada ya siku ya jumatatu.Mataifa mengi ya Magharibi ikiwamo Marekani tayari yameondoa wajmbe wao.
Siku ya ijumaa maelfu ya waandamaji walifanya maandamano katika bara bara za mji wa Tripoli na Benghazi kuwapinga wapiganaji ambao wamekuwa wakikabilian na vikosi vya serkali ya Libya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni