Kenya imekata rufaa ya mwaka moja iliyopewa kocha wa imu ya taifa Adel Amrouche na shirikisho la soka barani Afika CAF. amrouche alipigwa marufuku hiyo baada ya kudaiwa kumtemea mate afisa msimamizi wa mechi baina ya Harambee Stars ya Kenya na Comoros mwezi mei.
Katibu wa shirikisho la soka la Kenya FKF Michael Esakwa ameimbia BBC kuwa tayari wameshatuma ombi la kukata rufaa kwa shirikishi la CAF."baada ya kuona video ya tukio lilodaiwa kutokea baada ya mechi ninahakika kuwa hukuna aliyetamewa mate."
Sadfa ni kuwa kocho mkuu wa Comoros Amir Abdou amepuzilia mbali uwezekano wa tukio hilo akisema haiwezekani kuwa Amrouche alimtemea mate afisa huyo."mimi mwenyewe nilikuwepo na pia niliangalia video na kwa hakika ninaungana mkono FKF maana hii ilikuwa mechi ambayo tulishiriki.
Ujumbe huo wa kocha Abdou ulimpaga jeki Esakwa ambaye anasema kuwa taarifa hiyo itakuwa kati ya habari watakazopendekeza kutumiwa katika rufaa hiyo.
Kufuatia marufuku hiyo ya Amrouche, Kenya sasa inamtegemea kocha mbadala James Mandwa kuiongoza Kenya katika mechi ya mkondo wa pili ya kufuzu mechi ya kuwania dimba la mabingwa wa Afrika dhidi ya Lesotho, mechi hiyo itachezwa juma hili mjini Nairobi.
Kenya ilishindwa katika mkondo wa kwanza kwa kupigo cha bao moja kw nunge ugenini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni