GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumatatu, 22 Juni 2015

Mzee Majuto Amuunga Mkono Wema Sepetu, Diamond Amtaka Wema Abadilike Kama Kweli Anautaka Ubunge

 
Mzee Majuto  kwa mara ya kwanza ameamua kufunguka kumuunga mkono Wema Sepetu kwa nia yake ya kutaka kuwa mbunge.Kupitia ukurasa wake mtandaoni, Mzee Majuto ameandika;
Nisingependa kuyaongea haya kwenye mfungu mtukufu ila kiundani ningependa kuonyesha umoja na kumuunga mkono wazo na lengo la Mwanangu kwa kuwa anaweza na amethubutu sasa isitokee wale wasiopenda maendeleo ya watu na taifa hili kuvuruga misingi na mipango madhubuti ya kuwapa nafasi vijana na hasa wanawake kushika hatamu na kuleta mabadiliko.Kapeleke mabadiliko Singida na Tanzania nzima.

Muhimu ni kuwa na juhudi uwezo imani pamoja na uzalendo. Ujumbe huu pia ni kwa kila kijana na mwanamke mwenye lengo na nia ya udhubutu. Inshallah. Ramadhan Maqbul Waislam wote. Mzee Majuto alimaliza na kumtag Wema.

Moja kati ya waliochangia kwenye andiko hili la Mzee Majuto, ni Diamond Platnumz ambaye alimtaka Wema abadilike kama kweli anautaka ubunge.


  • “Swala siyo watu kumvunja moyo ,..ila yeye abadilishe akili ya mambo ya kushabiki migogoro ya watu wengine mitandaoni aache..katia aibu sana jana ,katangaza ubunge na bado ana shadadia ugomvi wa Diamond na Davido ,...mbunge ndo wakuwa na akili hii kweli,...watu wanahasira na upuuzi unaofanya na team yake na bado yeye mwenyewe anachochea ...watu watamuachaje....abadilike kama kweli anataka kugombea ubunge”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni