Swali la kwanza kabisa kuulizwa kwenye
Mdahalo wa Wakuu wa Vyama waliokutanishwa jana June 18 2015 Hyatt
Regency Hotel DAR, lilikuwa linahusu Changamoto ambazo wao wanaziona TZ…
Alikuwepo Prof. Ibrahim Lipumba, Zitto Kabwe, James Mbatia na Emanuel Makaidi ambapo mmoja mmoja alianza kutoa majibu ya swali hilohilo.
“Nchi za
Africa huwa tunabaki kulialia sana lakini lazima uangalie wenzako
Duniani kuna nini… Changamoto ya kwanza ni Katiba.. pili ni rasilimali
watu, changamoto nyingine ni tofauti zilizopo kati ya watu. Kuna tatizo
la umaskini, lazima pia tuwafanye Watanzania wajitambue.. Kwenye sekta
ya elimu hali ya Watanzania kufikiri iko chini sana”>>> James Mbatia
James Mbatia, Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi
“Katika
changamoto tulizonazo iko ya mama na wajawazito, katika kila watoto 100
chini ya miaka mitano, watoto 42 wana tatizo la udumavu. Changamoto ya
pili ni ukosefu wa ajira na tumeanza kuona matukio kama ya panya road,
watu wamepoteza matumaini kuishi kama binadamu wa karne ya 21.
Tatizo kubwa tulilonalo ni rushwa na ufisadi, lazima tuwaweke wala rushwa wote Segerea na sio kuchukua fomu za kugombea Urais”>>> Ibrahim Lipumba.
Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha CUF
“Ili nchi
iwe sawa lazima mzawa wa Tanzania apewe nafasi ya kwanza. Changamoto
nyingine ni ardhi, ardhi yetu nyingi inachukuliwa na wageni… Kingine ni
Uchumi wan chi hii umedorora, ukiona fedha inapungua thamani hii ni
dalili kwamba Uchumi unadorora. Changamoto nyingine ni afya, afya ya
Watanzania ni mbovu. Changamoto nyingine ni elimu, hata ukienda kwenye
midahalo na nchi nyingine utaona Mtanzania anapwaya” >>> Emanuel Makaidi.
Emanuel Makaidi, Mwenyekiti wa Chama cha NLD
“Changamoto
ya kwanza tuna Uchumi usiozalisha ajira, pili tuna huduma duni za
kijamii ikiwemo elimu, afya na maji… Changamoto ya tatu ni rushwa na
ufisadi, changamoto ya nne ni nyufa katika nchi yetu, nyufa za udini na
ukabila.. Yote haya tutayatatua kwa kuweka miiko ya Viongozi, huwezi
kuwa Waziri wa Kilimo na wewe ndio una zabuni ya kusambaza Mbolea, au
Waziri wa Maliasili na wewe ndio una vitalu vya kuwinda” >>> Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo
Majibu yao yako kwenye hizi sauti hapa, ukipla utawasikia wote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni