Askari Polisi wa Kikosi cha Tazara
jijini Dar es Salaam kinachosimamia ulinzi na usalama wa Reli ya
Tanzania na Zambia aliyetajwa kwa jina la PC Gineneko, ametekwa kisha
kuporwa bunduki aina ya SMG ikiwa na risasi 30 , Mei 27, mwaka huu.
PC Gineneko akiwa na majeraha baada ya kuvamiwa na majambazi.
Watekaji hao mara baada ya kumpora
bunduki askari huyo eneo la Yombo, Ilala jijini Dar es Salaam walitoweka
kusikojulikana.Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa watekaji hao
idadi yao inakisiwa kuwa sita na walijiandaa kufanya tukio hilo
kutokana na mazingira yalivyokuwa.
Shuhuda aliyesimulia tukio hilo huku
akiomba jila lake kuhifadhiwa kwa sababu za kiusalama, alisema ilikuwa
saa 12 jioni ambapo askari huyo alikuwa katika majukumu yake ya ulinzi
na wenzake na walipofika kwenye baa moja (jina linahifadhiwa)
walimkuta kijana anafanya biashara ya kuuza CD.
“Yule kijana mwenye CD akaanza kuzozana
na mwenzake, mmoja akadai kuwa amekuwa akimwibia CD zake na kwenda
kuuza sehemu nyingine, askari baada ya kuona mzozo umekuwa mkubwa
walikwenda kuwahoji kisa cha kugombana.
“Wakati vijana wale wakiendelea
kuhojiwa na askari, walitokea watu sita bila kujua walikuwa na lengo
gani, wakasema wanamtaka muuza CD , kabla polisi hawajakaa sawa,
vijana wale waliwazingira askari akiwemo aliyekuwa na bunduki ghafla
wakaanza kumshambulia kwa kumkata kwa panga na kumpora bunduki aina ya
SMG iliyokuwa na risasi 30 na kutomea.
Mfano wa bunduki aina ya SMG aliyoporwa.
Mmoja wa maafisa wa polisi ambaye si
msemaji, aliliambia gazeti hili kuwa mbinu waliyotumika majambazi wale
ni mzozo ulioanzishwa na wauza CD, hivyo kufanikisha tukio la uporaji
silaha.Katika tukio lingeni, jeshi la polisi kikosi hicho cha Tazara
wakati linasaka silaha hiyo, Juni 9, mwaka huu lilifanikiwa kukamata
bunduki nyingine maeneo ya Kwa Ally Mbowa baada ya kuwashitukia
majambazi watatu waliokuwa kwenye pikipiki.
“Askari wa doria (maarufu kama tigo)
walifanikiwa kuwadhibiti majambazi hao, mmoja alikamatwa na wananchi
wenye hasira wakampiga hadi kufa lakini bunduki aina ya AK 47 iliyokuwa
na risasi 13 ilipatikana,” alisema afisa huyo.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Reli, Tazara, SACP Patrick Byatao hakupatikana kufafanua matukio hayo licha ya kutafutwa kwa njia ya simu.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Reli, Tazara, SACP Patrick Byatao hakupatikana kufafanua matukio hayo licha ya kutafutwa kwa njia ya simu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni