Mwanzoni mwa mwezi huu kulikua na tetesi za chini chini kua Kanye West na mke wake Kim Kardashian walikua na mpango wa kubook Disneyland yote kwa ajili ya birthday ya mtoto wao wa kike North West aliekua
anatimiza miaka miwili. Tetesi hizo hazikua za uhakika sana ila kitu
cha uhakika ni hiki; wanafamilia hao walisherekea birthday ya mtoto wao
huko Disneyland Jumatatu 15 June na baadhi ya wanafamilia ikiwemo msanii wa HipHop Tyga na mwanae.
Hawakubook Disneyland kama tulivyosikia bali waliamua kwenda hapo kama watu wengine wa kawaida na kula good time huku wakienjoy birthday ya mtoto North West. Na kwa wale mafans wa Kanye West na Kim Kadarshian walipata nafasi ya kuwaona wanafamilia hao pamoja na kuwapiga picha bure bila Kanye West kuleta noma yoyote.
Hizi ni baadhi ya picha zilizoweka kwenye Instagram.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni