MSHTUKO! Mtoto
mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amezua gumzo ukumbini
baada ya kuonekana akiwa amevaa pete iliyoaminika kuwa ni ya uchumba na
kusababisha minong’ono miongoni mwa mashabiki wake.
Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Mpango mzima ulijiri wikiendi iliyopita
katika Ukumbi wa Sinema wa Mlimani City (Cinemax) kulipokuwa na uzinduzi
wa sinema ya 10 Bora ya washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talent,
mwaka jana ijulikanayo kama Mpango Mbaya.
Punde tu baada ya Lulu kuwasili ukumbini
hapo mishale ya saa mbili usiku akiwa na mashosti zake, minong’ono
iliibukia kwenye zulia jekundu wakati mrembo huyo alipokuwa akifotolewa
picha na mapaparazi ndipo wapenda ubuyu walipoanza kusambaziana habari
hali iliyosababisha watu wengi kutaka kumuona Lulu.
“Ile
ni ya uchumba aise atakuwa amechumbiwa, afadhali Lulu achumbiwe na
aolewe sasa japo bado anasoma lakini kwa kuwa ni chuo ni vyema na haki
akaendelea na uchumba wake huku akimalizia masomo na kisha ndoa
ikafuata,” alisikika mmoja wa mashabiki akiwaambia marafiki zake.
Baada ya watu kuanza kumzingira eneo
hilo kutaka kuishuhudia pete hiyo, haraka sana Lulu aliondoka eneo hilo
na kwenda kujibanza ukumbini kufuatilia sinema hiyo iliyokuwa imeshaanza
kuoneshwa.
Paparazi wetu alifanya jitihada za
kuzungumza na Lulu ili aweze kumsikia anazungumziaje pete hiyo
iliyopamba kidole chake lakini hakutaka kuzungumzia lolote akidai hayupo
tayari kufunguka lolote ukumbini hapo.
Hata baada ya muvi kuisha, paparazi wetu
aliendelea kumfuatilia Lulu wakati anatoka ukumbini lakini pia hakutoa
ushirikiano ambapo alionekana kukataa kupigwa picha pamoja na kujibu
maswali ya waandishi wa habari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni