Kiungo wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Chile Arturo Vidal
amekumbwa na mkasa ambao atapenda kuusahau haraka iwezekanavyo wakati
akiwa na timu yake ya taifa ambayo kwa mwaka huu imekuwa mwenyeji wa
michuano ya Copa America.
Vidal ambaye amekuwa kwenye kiwango bora tangu kuanza kwa michuano
hiyo akiwa amefunga mabao matatu kwenye mechi mbili amehusika kwenye
ajali ya gari ambayo imeelezwa kuwa yeye mwenyewe ndio alikuwa chanzo
cha ajali hiyo .
Vidal akiwa anaingia kwenye mazoezi ya timu ya taifa ya Chile akiwa na gari yake ambayo alipata nayo ajali jana.
Ripoti ya jeshi la polisi inasema kuwa Vidal alikuwa amelewa wakati
akiwa anaendesha gari aina ya Ferarri na alisababisha ajali ambayo
ilimsababishia majeraha madogo sambamba na mkewe .
Wote wawili waliwahishwa hospitalini ambako wamekuwa wakitibiwa huku
hali zao zikielezwa kuwa si mbaya kutokana na kupata majeraha madogo
kwenye ajali hiyo .
Gari la Vidal likiwa kwenye hali mbaya baada ya ajali .
Vidal alikuwa akitoka kwenye klabu moja ya usiku baada ya wachezaji
wa Chile kupewa ruhusu ya kuondoka kambini baada ya mchezo wao dhidi ya
Mexico.
Ripoti zaidi zinasema kuwa Vidal huenda akafukuzwa kambini ikiwa ni
moja ya hatua za kinidhamu toka kwa kocha wa timu ya taifa ya Chile
Jorge Sampaoli.
Nyota huyu anatarajiwa kupandishwa mahakamani hivi karibuni kujibu
mashtaka ya kuendesha gari akiwa ametumia kilevi na tayari ameporwa
leseni yake .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni