Kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la Al Qaeda, Mokhtar Belmokhtar aliyeuawa.
Kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la
kigaidi la Al Qaeda, Mokhtar Belmokhtar ameuawa katika mashambulizi ya
yaliyofanywa na Jeshi la Marekani nchini Libya.
Inasemekana kuwa, watu wengine kadhaa wameuawa wakati wa mashambulizi hayo.
Kwa upande wake, Wizara ya Ulinzi ya
Marekani kupitia Makao Makuu ya Jeshi la nchi hiyo (Pentagon) imedai
kuhusika na mashambulizi hayo wakikusudiwa kumlenga gaidi huyo (Mokhtar
Belmokhtar) wa mtandao wa Al Qaeda.
Kanali Steve Warren, msemaji wa Pentagon
amesema kuwa, mashambulizi hayo yalifanywa Jumamosi usiku na kwamba
hivi sasa wanatathmini matokeo ya oparesheni yao hiyo.
Blmokhtar anaaminika kuwa ndiye
aliyeongoza shambulizi kubwa la kigaidi katika kiwanda cha gesi nchini
Algeria mwaka 2013, shambulzi lililosababisha vifo vya watu 35 wakiwemo
raia watatu wa Marekani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni