LANDOVER,
MD – JUNE 07: Iker Casillas of Spain comes off by David de Gea of Spain
during an international friendly match between El Salvador and Spain at
FedExField on June 7, 2014 in Landover, Maryland. (Photo by David
Ramos/Getty Images)
Huku taarifa zikizidi kumiminika kuhusu kllabu ya Real Madrid
kukaribia kumsajili kipa David De Gea wa Manchester United , taarifa
nyingine zimeibuka zikimhusisha kipa namba moja wa klabu hiyo Iker
Cassilas na kuihama klabu hii ambayo ameitumikia kwa muda mrefu .
Cassilas inasemekana kuwa amefikia uamuzi wa kuondoka klabuni hapo
ili kuepusha tatizo ndani ya klabu hiyo linaloweza kusababishwa na vita
ya kuwania namba kati yake na David De Gea wakati kipa huyu wa zamani wa
Atletico Madrid atakaposajiliwa .
Real Madrid tayari imefikia uamuzi wa kumsajili De Gea na ishara zote
zinaonyesha kuwa kipa huyu anaelekea kuwa kipa namba moja ndani ya
Santiago Bernabeu na Cassillas ambaye kwa miaka ya hivi karibuni amekuwa
akicheza chini ya kiwango chake cha kawaida amejiandaa kuondoka .
Ripoti iliyonukuliwa toka kwenye Televisheni ya Taifa ya Hispania
inasema kuwa Real Madrid imemuandalia Cassilas mchakato wa kuihama klabu
hiyo kwa heshima kwani inathamini mchango wake .
Cassillas alianza kuitumikia klabu hii tangu akiwa na umri mdogo
ambapo alipata nafasi ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza akiwa na umi
wa miaka 19 akicheza kwenye fainali ya ligi ya mabingwa ambapo aliingia
kuchukua nafasi ya kipa aliyeumia .
Cassillas amekuwa kipa namba moja kwa muda wote tangu alipoanza
kuingia kwenye kikosi cha kwanza akitokea kwneye kikosi cha vijana na ni
misimu miwili iliyopita pekee wakati alipopoteza nafasi yake kwa kipa
Diego Lopez kufuatia jeraha alilopata .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni