Jengo la kituo cha Radio kilichochomwa moto Burundi.
Kama ulipitwa na hii Breaking News kutoka Bujumbura Burundi asubuhi ya May 14 2015 zilitoka taarifa kwamba raia hawatoki nje, milio ya risasi inasikika, Wanajeshi watiifu wa Rais wanapambana na waliotangaza kumpindua jana.
Pia kituo binafsi cha Radio kilichotumika kutangaza mapinduzi ya kijeshi kilichomwa moto saa tisa usiku wa kuamkia May 14 2015 na Wanajeshi wanaomtii Rais lakini hakuna yeyote aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha.
Wa kwanza kushoto ndio Jenerali mwenyewe aliyetangaza mapinduzi, hapa
ndio alikua anaondoka kwenye jengo hilo muda mfupi baada ya kutangaza
mapinduzi.
Jengo la Radio kabla ya kuchomwa moto.
Hii picha ni wakati Meja Jenerali Godefroid Niyombareh akitangaza mapinduzi hayo kwenye Radio.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni