Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la ajali za pikipiki na kugharimu maisha ya watumiaji wa usafiri huo tangu Serikali ilipoidhinisha matumizi ya vyombo hivyo mwaka 2009 ambapo ongezeko hilo limesababisha hasara ya shilingi trilioni tatu kutokana na matibabu kwa majeruhi na uharibifu wa miundombinu ya barabara.
“… Kutokana na ajali hizo inakadiriwa kwamba Taifa limepoteza zaidi ya shilingi trilioni 3.2 mwaka jana tuu… kwa maana ya uharibifu wa vyombo vingine vya usafiri, uharibifu ya miundombinu , gharaza za matibabu na bima, gharama za uokoaji na usimamizi, upotevu na uharibifu wa mali kwenye magari husika na Sumatra nawaombeni sana hebu washirikisheni wenzenu trafiki wale… Kamanda Mpinga anzisheni jamani uhusiano wa karibu na waendesha pikipiki kupitia asasi yao hii sasa ya mafunzo hii ya APEC… hebu kuweni karibu sana... ”– Waziri Mwakyembe.
Nilikurekodia sauti wakati habari hiyo ikiripotiwa na kituo cha TBC 1, unaweza kubonyeza play kuisikiliza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni