GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumanne, 16 Desemba 2014

Ni dili juu ya dili kwa Lupita Nyong’o. Katuhakikishia 2015 bado ni mwaka wake

354645b2afb9c9365da23d9412bad7cd

Staa ambaye huenda anaongoza kutokea kwenye headlines nyingi zaidi za vyombo vya habari vya Kimataifa akiwakilisha 254, Lupita Nyong’o ameendelea kung’aa na kwa hii ya leo ni ishara tosha kwamba 2014 ulikuwa wa neema kwake na bado 2015 una dalili zote za neema kendelea kumshukia staa huyo.

‘12 Years a Slave‘ ilimfungulia njia nzuri ya Dunia yote kumfahamu, baada ya hapo deal kibao zimemuangukia ikiwa ni pamoja na za uanamitindo ambapo ameshakusanya tuzo kadhaa ikiwemo ile ya mwanamke mzuri zaidi duniani na tuzo ya Oscar.

Deal mpya ni kwamba anatarajia kuingia location muda wowote kuanzia sasa kwa ajili ya kushoot movie mpya ya ‘Americanah’ ambayo atakuwa staa akishirikiana na David Oyelowo  ambapo movie hiyo ni story iliyotokana na novel ya ‘Chimamanda Ngozi Adichie’ kilichoandikwa Nigeria.
Kampuni ya Brad Pitt ambayo ilitayarisha movie ya 12 Years a Slave inahusika kuitayarisha hii pia, hakika baada ya zile Oscar na Glamour awards, kuna dalili ya tuzo nyingine kumwendea iwapo akipiga kazi poa mwaka 2015 kama ilivyokuwa mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni