GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumanne, 16 Desemba 2014

Kama hukupata nafasi ya kusikiliza 255 ya kwenye XXL ya leo December 16 nimekuwekea hapa

mp,550x550,matte,transparent,t.3

Kwenye 255 ya XXL   msanii Q Chillah amezungumza kuhusu namna alivyokutana na Management yake mpya  ambayo moja ya malengo yake ni kumtambulisha msanii huyo upya pamoja na kuyabadili maisha yake.

Kwa sasa tayari wameshaanza kufanya kazi na wimbo mmoja ambao wameamua kuutumia kumtambulisha Chillah upya kwenye game tayari umerekodiwa na wako kwenye mikakati ya kufanya video yake Afrika Kusini, ambapo ataitambulisha kwanza nyimbo hiyo kabla ya kwenda kurekodi video yake Afrika Kusini.

Rapa Young Killer amesema kwamba hana uhusiano wowote wa kimapenzi na msichana Halimati ila wanafahamiana kwa kipindi kirefu tangu kipindi ambacho rapper huyo hajatoka na kufahamika.

Mwanzoni mwa mwezi huu kulikuwa na tetesi kuwa  rapper Wiz Khalifa amerekodi mkanda wa ngono na model wa magazine ya Playboy Magazine, ambapo msanii huyo alikataa kusign ili mkanda huo kusambaa mtaani,  lakini inasemekana kuwa  Kampuni inayoongoza kwa kununua mikanda ya aina hiyo ya watu maarufu  imetangaza dau kubwa ambalo huenda likamvutia Wiz akasign deal hiyo.

Nick Minaj amekuwa akizushiwa kutoka na mastaa kadhaa tangu aachane na mpenzi wake  ambapo safari hii amekanusha ule uvumi kwamba ana uhusiano wa kimapenzi Meek Mill.
Unaweza kuisikiliza 255 hiyo kwa kubonyeza play hapa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni