Nahodha wa Chelsea, John Terry ameisaini jezi yake ya mechi na kuituma kwa mmoja wa mashabiki wa Chelsea aliyefiwa na mama yake.
Shabiki huyo alitumiwa ujumbe na Terry kupitia mtandao wa kijamii akimuambia kuwa amemtumia zawadi hiyo ya jezi kumfariji.
Terry aliandika: Pole sana taarifa za majonzi kuwa mama yako amefariki dunia.
Ningependa kutuma moja ya jezi zangu kwa ajili ya mechi na kuweka saini yangu ili ujue mimi na Chelsea tuko pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu.
Baadaye shabiki huyo aitwaye Louise alituma kwenye Instagram akionyesha jezi hiyo baada ya kuipokea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni