GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumapili, 7 Septemba 2014

Mgonjwa Aliyekuwa Akiombewa Kanisa la Gwajima Akutwa Amefariki Gesti


Habari mbaya inamhusu mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Averina ambaye alikuwa akiombewa kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima la Nabii Josephat Gwajima ambaye anadaiwa kufia nyumba ya kulala wageni (gesti) ya My Fair iliyopo Kawe jijini Dar.

Tukio hilo lililoacha viulizo na kuzua minong’ono midomoni mwa wengi lilijiri hivi karibuni ambapo mwanadada huyo aligundulika kuwa amefia chumbani mishale ya saa 4:00 asubuhi.

Akizungumzia tukio hilo, mlinzi wa gesti hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Haruni alisema, mwanamke huyo alifikishwa mahali hapo akionekana dhaifu kiafya, jambo lililosababisha kumuhoji mtu aliyemfikisha hapo kuwa ni kipi kimemsibu.

“Huyu dada alipofikishwa hapa na mtu ninayemfahamu ambaye nasali naye kanisa moja la Sabato, nikalazimika kumuhoji mama huyo aliyemleta ana matatizo gani na kwa nini wamlaze gesti wakati ni mgonjwa, ndipo akanipa mkasa mzima.

“Aliniambia huyu mama hana makazi maalum na alikuwa akisali kwa Gwajima na kulala uwanjani hapo (Tanganyika Parkers, Kawe) huku hali yake ikiwa si nzuri kiafya,” alisema mlinzi huyo.
Aliendelea kusema kwamba hadi kufikia uamuzi wa kumlaza mahali hapo ni baada ya kuona hana makazi huku akisaidiwa kupata matibabu.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa gesti hiyo, Apolinary Shayo alisema siku ya tukio alipewa taarifa kuwa kuna mtu amefia ndani na alipojaribu kumuhoji mtu aliyekuwa ameenda naye kwa kuwa alikuwepo mahali hapo kwa lengo la kumpelekea chakula mgonjwa wake, akamueleza kuwa mama huyo alikuwa akisumbuliwa na magonjwa tofauti (hayakutajwa) kwa muda mrefu.

Mwili wa mwanamke huyo ulichukuliwa na polisi wa Kituo cha Kawe, Dar kwa uchunguzi zaidi na kutafuta ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi ikidaiwa kwamba mama huyo alitokea mkoani (haikujulikana ni mkoa gani).


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni