GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumapili, 7 Septemba 2014

Mdogo wa Flora Mbasha Aeleza Mahakamani Jinsi Mbasha Alivyombaka


Shahidi wa kwanza katika kesi ya kubaka inayomkabili mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha, ameieleza mahakama jinsi mshtakiwa alivyomkaba shingo na kumziba mdomo kwa kutumia nguo, kisha kumbaka.

Shahidi huyo ambaye ni shemeji yake, mwenye umri wa miaka 17, aliyasema hayo jana wakati akitoa ushahidi wake katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala.

Hata hivyo, kesi hiyo ilisikilizwa kwa faragha(Chamber Cort) baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali Nassoro Katuga kuiomba mahakama kesi hiyo kuendeshwa kwa faragha kwa kuwa imefikia hatua ya kusikilizwa na sheria inaonyesha kuwa mtoto huyo yupo chini ya miaka 18.

Ombi hilo lilikubaliwa na pande zote mbili na kesi hiyo kuendeshwa katika mahakama ya faragha na Hakimu, Wilbaforce Luhwago aliomba watu wote walikuwepo ndani ya mahakama hiyo kutoka nje ili kupisha upande wa mashtaka kutoa ushahidi.

Akiongozwa na mwendesha Mashtaka wa Serikali Nassoro Katuga, shahidi huyo alidai siku ya tukio, Mei 23, mwaka huu, mshtakiwa aliondoka na mke wake kwenda kufuatilia mkanda wa video lakini ghafla alirudi nyumbani kwake Tabata Kimanga akiwa peke yake.

Alidai siku hiyo ya tukio mshtakiwa alifanikiwa kufanya mapenzi na binti huyo na kumwambia asimwambie mtu wakati mke wake akiwa hayupo nyumbani hapo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 12,2014.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni