GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumatatu, 1 Septemba 2014

DIAMOND ALIVYOOKOLEWA NA POLISI WA UJERUMANI KUTOKA KWA MASHABIKI WENYE HASIRA

Stuttgart,Ujerumani,

Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,Ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.
Washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake Mr.Awin Williams Akipomiemie raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
Hapo ndipo washabiki hao walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake,
Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki
ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.
Moja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ  Flor alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo  DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. 
Polisi nchini Ujerumani wamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea,kwani msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari sana,kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa
wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.

Hivi ndivyo ukumbi huo ulivyokuwqa baada ya tafrani hiyo.
Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wana hasira nawe DIAMOND"  link:
http://www.stuttgarter-nachrichten.de/inhalt.blaulicht-aus-der-region-stuttgart-31-august-diamond-platnumz-zieht-aerger-der-fans-auf-sich.ca1f4b9d-599b-4c95-84c8-fe25d10b6ed9.html

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni