GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumapili, 10 Agosti 2014

RAILA ADAI ANAJUA WALIOTEKELEZA MAUAJI MOMBASA

Raila Odinga

KIONGOZI wa Muungano wa Cord Raila Odinga amedai kwamba anawajua watu waliohusika katika mauaji ya majuzi katika Mombasa, na kusema walitumiwa na serikali.

Aidha, alipuuzilia mbali Waziri wa Ardhi Charity Ngilu na kusema kwamba hana mamlaka ya kuingilia suala la ardhi nchini.

Akiongea Jumapili katika Kanisa la Ushindi Baptist, Likoni, alidai waliotekeleza mauaji waliagizwa wafanye hivyo na serikali. Alisema ana majina ya wote waliohusika.

“Ni jambo la kuhuzunisha kwamba Wakenya waliuawa. Serikali hii imeshinda katika jukumu lake la kudumisha usalama,” akasema Bw Odinga.
Kuhusu ardhi, alisema vitendo vya Bi Ngilu ni vya kutilia shaka akidai kwamba lengo lake ni kunyakua ardhi zaidi.

“Bi Ngilu anafaa kuacha makarani wa sajili za ardhi wafanye kazi yao. Tutamsamehe kwa kuwa alikuwa karani tu. Hiyo ndiyo kazi aijuayo vyema zaidi,” akasema.

Bw Odinga alisema pia kwamba jukumu la kubatilisha ekari 500,000 za ardhi Lamu ni la Tume ya Kitaifa ya Ardhi (NLC) na si Waziri wa Ardhi.

“Hatuwezi tukaruhusu fisi asimamie mbuzi hali twajua kwamba katiba haimruhusu Bi Ngilu kusimmaia masuala ya ardhi,” akasema.

Kuhusu usalama Lamu, Bw Odinga alisema serikali ilinoa kwa kumkamata na kumfungulia mashtaka Gavana wa Lamu Issa Timammy bila kufanya uchunguzi.

“Inakuwaje kwamba hawajawahi kumshtaki na bado wanamchunguza kama walikuwa na ushahidi kumhusu?” akauliza.
Kadhalika, Bw Odinga alitoa wito kwa Wakenya kukoma kujihusisha katika uhasama wa kidini.

Chanzo: Swahili Hub

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni