GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Ijumaa, 8 Agosti 2014

Mshukiwa wa al-Shabaab aliyekamatwa Kenya kupelekwa Somalia

Kenya imekubali ombi la Somalia la kumrejesha raia mmoja wa Somalia anayeaminika kuwa mjumbe wa ngazi za juu wa al-Shabaab, Hassan Haji Hanafi, afisa mmoja wa Somalia aliiambia Sabahi siku ya Alhamisi (tarehe 7 Agosti).

Balozi wa Somalia nchini Kenya, Mohammed Ali Nur, aliiambia Sabahi kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa tarehe 3 Agosti kwenye kiunga cha Eastleigh, Nairobi, kutokana na kutuhumiwa kuhusika na mauaji ya waandishi wa habari wa Kisomali.

"Uwezekano wa kuwa yeye ni Hassan Haji Hanafi ni mkubwa sana licha ya kudai kwake yeye siye," alisema Nur, akiongeza kwamba mtu huyo anayeaminika kwamba ni Hanafi alikuwa Kenya kwa ajili ya matibabu maalum kwa majeraha "yanayoonekana kutokana na mapigano."

"Kwa kuwa uhalifu aliokamatiwa ulitendeka Somalia, tuliiomba serikali ya Kenya kumsafirisha kwenda Somalia kwa ajili ya uchunguzi zaidi na [kumtambua]," alisema. "Tumefurahi kwamba Kenya imelikubali ombi letu kwa sababu ni sisi pia tuliomba akamatwe."

Nur alisema mtuhumiwa huyo angelirejeshwa Somalia mara tu mamlaka nchini Kenya zitakapokamilisha uchunguzi wao wenyewe.

Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, hakujibu ombi la Sabahi juu ya maoni yake kuhusu makubaliano hayo ya kukamatwa na kusafirishwa kwa mtuhumiwa huyo.

-Sabahi