Mkutano wa 6 wa Kamati ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kenya umeanza leo hapa mjini Tehran, na unawakutanisha wataalamu wa pande mbili.
Mkutano huo utahudhuriwa hapo kesho na Muhammad Hujjati Waziri wa Jihad ya Kilimo wa Iran atakayeongoza timu ya Iran na Bi. Amina Muhammad Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Kenya anayeongoza timu ya serikali ya Nairobi.
Inatarajiwa kuwa, katika siku ya pili ya mkutano wa Kamati ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran na Kenya, maafisa wa pande mbili watajadili masuala mbalimbali na kutia saini hati kadhaa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.
-IRB
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni