Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) imeahidi kutoa msaada wa dola milioni 1 ili kusaidia jitihada za kuzuia kuenea ugonjwa wa Ebola katika nchi za Magharibi mwa Afrika.
Afisa wa AU anayeshughulikia masuala ya kijamii Mustapha Sidiki Kaloko amesema kuwa, kamisheni ya AU imajizatiti kuhakikisha kwamba hatua zinachukuliwa ili kuzuia kuenea zaidi homa ya Ebola barani Afrika.
Matamshi hayo yametolewa huku Umoja wa Afrika ukitoa wito wa kuimarishwa mifumo ya ufuatiliaji pamoja na utoaji elimu kwa jamii ili kuzuia kuenea virusi vya homa ya Ebola.
Nchi 54 wanachama wa AU pia zimepanga kufanya mkutano wa mawaziri mwezi ujao kujadili masuala ya afya ili kuhuisha Mfuko wa Maalumu wa Dharura kwa ajili ya Ukame na Njaa ambao pia unajumuisha masuala ya afya ya jamii.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) homa ya Ebola tayari imeua watu 1,145 huko magharibi mwa Afrika katika nchi za Liberia, Guinea, Sierra Leone na Nigeria.
-IRB
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni