GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumatatu, 11 Agosti 2014

Madawa ya kulevya yamtesa tena Agness Masogange...... Abadili Uraia.

Masogange baada ya kuchomoka kwenye ule msala wa awali wa madawa ya kulevya, video queen matata Bongo, Agness Gerald 'Masogange'  amejikuta akiteseka sana kwa ishu hiyo kwa mara nyingi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia GennSwahili, Masogange alipatwa na msala huo baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam Tanzania hivi karibuni akitokea nchini Afrika Kusini 'Sauzi' ambako alidakwa na polisi wa kitengo cha madawa ya kulevya nchini kilichopo chini ya Godfrey Nzowa.

Akisimulia  ishu hiyo , Msogange ambaye umaarufu wake mkubwa ulizaliwa katika Video ya Abednigo Damiani 'Bell 9' alisema alikamatwa na watu wa uhamiaji nchini baada ya kuhisiwa kuwa hati yake ya kusafiria ina matatizo.

"Walinikamata baada ya kuona hati ilikuwa na ule msala wa awali lakini walinihoji na nikiwapa majibu ambayo yaliwaridhisha , wakaniachia.

"Hii ishu inantesa sana lakini namshukuru Mungu kwa kuwa nakamilisha taratibu za kuwa Raia wa Afrika Kusini,nitaishi kule" alisema Masogange alipobanwa na Risasi Jumamosi.

Juzi kati wakati gazeti hili ilikwenda mitamboni, Masogange alikuwa kwenye Ubalozi wa Sauzi nchini katika harakati a mwisho kukamilisha taratibu za kuwa NA Uraia wa Afrika Kusini ambako alisema ndiko atakapokuwa akiishi.


Julai 9 mwaka jana, Masogange alikamatwa na madawa ambayo yalihisiwa kuwa ya kulevya nchini Afrika Kusini akashikiliwa na polisi kwa miezi kazadhaa.

Septemba , mwaka jana Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesbug, baada ya uchunguzi kukamilika na kubaini  hayakuwa madawa ya kulevya bali ni chemikali zinazotengenezea madawa ya kulevya,Masogange alitakiwa kulipa faini ya R30,000 (Tsh 4.8 Milioni) akawa huru,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni