Mtendaji Mkuu wa Barclays PLC, Anthony Jenkins akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC Tanzania wakati wa ziara yake nchini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Bi. Mizinga Melu.
Mtendaji Mkuu wa Barclays PLC, Anthony Jenkins (kulia) akipozi kwa picha na Rachel Mwalukasa mmoja wa wafanyakazi aliyemkabidhi tuzo kwa kuwa mfano wa kuigwa katika suala la kujitolea binafsi katika kuisaidia jamii. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji nwa NBC Tanzania, Mizinga Melu.
Wafanyakazi wa NBC Tanzania wakionyesha sura ya matumaini wakati wakimsikiliza bosi wao, Antony Jenkins alipokuwa akizungumza kuhusu mikakati ya kimaendeleo ndani ya benki hiyo nchini.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC wakishangilia hotuba ya Mtendaji Mkuu wa Barclays PLC, Anthony Jenkins wakati wa ziara yake nchini Tanzania.
Wafanyakazi wa NBC Tanzania wafuatilia kwa makini hotuba ya Mtendaji Mkuju wa Barclays PLC, Anthony Jenkins wakati wa ziara yake nchini ambapo alifanya mikutano na wafanyakazi, wateja wa NBC na wadau wengine wa benki hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni