Staa wa filamu za Kibongo,Wema Sepetu ametajwa kuwa ndiye aliyechangia
kwa kikubwa ushindi wa tuzo tano za Killi za msanii wa Bongo Fleva,Ali
Kiba kutokana na kumpigia debe mara nyingi kupitia akaunti yake ya
Instagram.
Akifunguka kupitia 255 ya XXL,Wema alisema kuwa Ali Kiba alimuomba ampigie debe kwenye akaunti yake ya Instagram,kwani hata msanii huyo aliwahi kumpigia debe alipowania tuzo za Watu ndiyo maana alifanya hivyo.
Hata hivyo alipoulizwa mbona hakumpigia debe aliyekuwa mpenzi wake,Diamond Platinum ambaye ni hasimu wa msanii Ali Kiba,alisema kuwa Diamond hakuwahi kumuomba ampigie debe kama angemuomba angefanya hivyo kwani hana tatizo na msanii huyo.

- ‘’Sina tatizo na Diamond kama angeniomba nimpigie debe Instagram ningefanya hivyo,’alisema Wema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni