
Stori ya Msiba wa aliyekuwa Sheikh Mkuu Tanzania, Mufti Sheikh Issa Shaaban Bin Simba imechukua nafasi kubwa sana kwa kuripotiwa kwenye vyombo vingi vya Habari.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum nimemnukuu akithibitisha juu ya msiba huo >>> “Ni
kweli Mheshimiwa Mufti amefariki.. Kesho saa nne asubuhi Waislamu na
Viongozi wote watajumuika Makao Makuu ya BAKWATA, Kinondoni Muslim
kuuaga mwili wa Sheikh. Mchana mwili wa Sheikh utasafirishwa kwenda Shinyanga, atazikwa siku ya Alhamisi“>>>– Sheikh Alhadi Mussa Salum
Hapa anamzungumzia Marehemu Mufti Simba>>> “Mufti
alikuwa na sifa ya kuwa Kiongozi wa Waislamu. Alikuwa mvumilivu sana
na msamehevu katika Utawala wake. Angekuwa hana subira Waislamu
wasingekuwa na uvumilivu“>>>– Sheikh Alhadi Mussa Salum

Hapa nina sauti niliyomrekodi Sheikh Alhadi Mussa Salum akizungumzia msiba huo na akimzungumzia Marehemu pia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni