
Kuna mtu unaweza kumzungumzia mambo yake binafsi akakaa kimya tu
asiongee lolote lakini wengine huwa hawapendi kabisa.. ishu ya
kuongelewa madeni yake kwenye Kikao cha Bunge, Mchungaji Peter Msigwa hakuipenda.
“Nampongeza Waziri wa Fedha, kwa kweli anafanya kazi yake vizuri.. Nchi hii iko taabani fedha hakuna lakini Waziri bado yumo tu.
Na hata Msigwa angepewa Wizara hii kama
fedha isingekuwepo nae angekuwa hoi vilevile… Sasa Msigwa anashangaa
Serikali inadaiwa yeye mwenyewe juzi kaletewa makaratasi anadaiwa…
Kudaiana ni jambo la kawaida“>>>– Mbunge Said Mtanda.
Mbunge Peter Msigwa akawasha kipaza sauti; “Mbunge
anaezungumza anaingilia mambo binafsi, masuala ya madeni yangu
asiyajadili hapa. Hili ni Bunge tunajadili mambo ya Nchi, anajuaje
madeni yangu? Huku ni kuniingilia, aache kabisa kuingilia mambo yangu”>>>– Mbunge Peter Msigwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni