
Nigeria ni moja ya nchi ambazo ziko
kwenye wakati mgumu sana kutokana na mashambulizi ya Kigaidi, stori
nyingine kwenye Headlines kutoka huko inahusu ishu ya mlipuko wa mabomu
ambao umesababisha vifo vya watu 63 Jimbo la Borno.
Mabomu hayo ni kama yalisahaulika au
yalitelekezwa hivi, vijana walikuta begi likiwa na milipuko hiyo katika
eneo ambalo Boko Haram waliwahi kuweka Kambi yao, wakalibeba begi hilo
mpaka eneo ambalo kuna watu wengi ambao walizunguka kulishangaa… muda
mfupi baadae mabomu hayo yalilipuka.
Katika watu 63 waliofariki wengi wao ni
vijana wa kiume na wanawake ni wachache, wapo wengine wengi ambao
walipata majeraha pia kwenye tukio hilo.
Polisi wamelaumu kitendo cha watu hao
kukuta milipuko hiyo na kukaa nayo bila kutoa taarifa Polisi au kwenye
Kikosi cha Jeshi ambao wangeweza kuishughulikia kabla ya kuleta maafa
hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni