
Mastaa na maisha yao nyuma ya pazia, mengine ni haya nimeyajua leo toka kwa wakali wa Nigeria, Peter na Paul watoto wa Marehemu Chief Moses Okoye… wamesema toka mwaka 2007 hawaendi kanisani, kisa unajua ni nini?
Jamaa hao ambao kwa pamoja dunia inawajua kama P Square
wameingia kwenye Headlines baada ya kufanyiwa Interview na kuyafunua
mengine kwamba hawajaenda Kanisani toka mwaka 2007 kwa vile ilikuwa
wakiingia tu macho ya watu wote yanakuwa kwao!!
“Kila mara
tukiingia Kanisani macho ya watu wote yanakuwa kwetu, wanaacha
kumsikiliza Mchungaji.. wanaacha kusali wanaanza kutushangaa“>>> P Square.

“Tuliona sio vizuri.. ni kama tulikuwa
tunasababisha watu waache kufanya kilichowapeleka Kanisani, tukaamua
tuache kabisa kwenda Kanisani… Watu wote ni sawa mbele za Mwenyezi
MUNGU, sio kitu kizuri watu wakasahau kusali kwa sababu yetu”—P Square.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni