
Musa mateja
NInoma! Kumbe lile gari la kifahari aina ya BMW ambalo muigizaji nyota wa filamu Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ alizawadiwa wakati wa bethidei yake na kuwa miongoni mwa sababu za kumwagana na mpenzi wake wa awali, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ mwaka jana, linadaiwa kuwa kimeo kwa vile limekuwa likiharibika mara kwa mara, Amani lina stori kamili.
Gari aina ya BMW la Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Mapema wiki hii, paparazi wetu alikuta gari hilo likiwa limebuma
mitaa ya Victoria, Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku mshindi huyo wa
Shindano la Miss Tanzania mwaka 2006 akiwa ndani, lakini ili kukwepa
aibu, aligoma kutoka nje kuomba msaada, badala yake akabakia ndani huku
akijaribu kuwasiliana na watu wake wa karibu.
Mmoja wa wasaidizi wake wa karibu, Petit Man baadaye akitumia gari jingine alifika eneo hilo akiwa ameambatana na fundi, ambao walilisukuma hadi eneo salama na kuliegesha. Wema alibakia ndani ya gari hilo wakati fundi akijaribu kurekebisha dosari ambayo haikuweza kufahamika mara moja.
Wema akiwa ndani ya gari hilo.
Hadi gazeti hili linaondoka eneo hilo baada ya juhudi za kumpata ili
azungumze kugonga mwamba, hakukuwa na dalili za kupatikana kwa
ufumbuzi.Mtu wa karibu na Madam aliliambia gazeti hili kuwa gari hilo
limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu kiasi kwamba wakati mwingine
hulikumbuka gari aina ya Nissan Murano, ambalo alipewa na Diamond siku
hiyohiyo ya bethidei yake, lakini akaliuza baada ya wawili hao
kutofautiana.

Baadaye
Wema alitafutwa kupitia simu yake ya mkononi, lakini haikuweza
kupatikana ili azungumzie juu ya gari hilo, ingawa siku za nyuma wakati
gari hilo lilipokutwa likiwa limetolewa matairi eneo la Komakoma,
alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa anahisi BMW hilo lilikuwa
limetumika sana kabla ya kupewa kwa vile limekuwa likimsumbua mara kwa
mara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni