GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumamosi, 17 Januari 2015

EPl: Matokeo ya Chelsea vs Swansea na Liverpool vs Aston Villa haya hapa

IMG_0988.JPG

Ligi kuu ya England imeendelea jioni ya leo Katika viwanja tofauti nchini humo.
Viongozi wa ligi Chelsea walisafiri mpaka Cardiff kwenda kucheza na Swansea City ambao wameondokewa na mchezaji wao tegemezi Wilfred Bony aliyehamia Manchester City.
Matokeo ya mchezo huo ni ushindi mnono kabisa kwa Chelsea mwaka huu, wakishinda 5-1.
Magoli ya Oscar na Diego Costa katika kipindi cha kwanza yaliipeleka Chelsea mapumziko wakiwa wanaongoza 4-0 – Oscar na Costa wakifunga mara mbili mbili kila mmoja.
Kipindi cha pili dakika ya 80 Andre Schurrle alifunga goli la tano na kuhitimisha kalamu ya magoli ya Chelsea.
Huko Villa Park – Liverpool wameendelea kupata matokeo chanya baada ya kuifunga Aston Villa 2-0.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni