Mabingwa wa England, Manchester City wameanza kuonja joto ya jiwe wa Ligi Kuu England baada ya leo kulala kwa bao 1-0.
Stoke City ambao waliinyanyasa Man City msimu uliopita, leo ‘wameifanyia mbaya’ kwa kuichapa kwa bao 1-0 tu.
Mame Diouf ndiye alikuwa shujaa wa Stoke City waliokuwa nyumbani baada ya kuwapangua viungo na mabeki wa wageni wao kabla ya kupachika bao akipiga mpira uliompita kipa Joe Hart katikati ya miguu yake, unaweza kusema topo.
Juhudi za Man City kutaka kuchomoa 'kashfa' hiyo ziligonga mwamba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni