GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumatano, 25 Juni 2014

Suarez amng'ata Chiellini

   
.  

Mshambulizi wa Uruguay Luis Suarez amekumbwa na kashfa mpya baada ya kuonekana kumngata Giorgio Chiellini wa Italia.
Suarez alionekana akiminya bega la Chiellini muda mchache kabla ya Diego Godin kufunga bao la ushindi la Uruguay dhidi ya Italia.Chiellini aliangushwa chini na uchungu wa meno ya Suarez na alionekana akimkimbilia refarii akimvulia shati ilikuonesha alama ya meno begani lakini refarii akapuzilia mbali .
Chiellini ameiambia runinga moja ya Italia kuwa Suarez alijiangusha chini likuficha uovu huo wa kutisha na kusingizia kuwa alikuwa amepigwa kumbo.Suarez alionekana akigaaga uwanjani baada ya tukio hilo.
Japo refarii Marco Rodriguez hakuona tukio hilo la kutamausha Chiellini amesikika akisema kuwa ni jambo la kuhuzunisha kuwa refarii huyo alipuzilia mbali maombi yake ya kutaka hatua ichukuliwe dhidi ya mshambulizi huyo ambaye aliadhibiwa kwa tukio lengine kama hilo akiichezea Liverpool misimu miwili iliyopita nchini Uingereza.
Suarez alilazimika kukaa nje kwa mechi 10 baada ya kumngata kiungo wa Chelsea Branislav Ivanovic aprili 2013.
  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni