Mwaka 2009 Kenya waliingia kwenye
Headlines kuhusu ishu ya Ikulu ya nchi hiyo kununua magari ya kifahari
na ikawa skendo kubwa sana kwa vile wakati magari yananunuliwa Rais Mwai Kibaki alikuwa
likizo wakati huo… Bunge la Tanzania imesikika pia ishu ya kulalamikiwa
kuhusu Serikali kutumia magari ya kifahari, stori iko tofauti sana toka
Ugiriki.
Yanis Varoufakis
ni Waziri wa Fedha wa Ugiriki, jamaa hata hana mambo mengi yani..
haitaji kuzinguana kwenye foleni barabarani wala nini, usafiri wake
kwenda Ofisini ni pikipiki aka bodaboda !!
Ready to go !!! Hapo safari inaanza toka Ofisini.
Waziri sio mchoyo, kampa lift Euclid Tsakalotos ambae ni Naibu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Kiuchumi wa Ugiriki.
Mheshimiwa Waziri kafunguliwa geti anaingia zake Ofisini mdogomdogo !!
Kiutaratibu kabisa Kiongozi wa nafasi
yake anatakiwa awe kwenye gari na awe na dereva wa kumwendesha, lakini
huu ndio usafiri wa chaguo la moyo wake kabisa mtu wangu !!
Unaona kuna viongozi TZ wataweza maisha kama hayo mtu wangu?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni